Waziri wa Habari na Utamaduni wa nchini Nigeria Alhaji Lai Mohammed asubuhi ya leo March 21, 2018 ametangaza kuwa kikundi cha Wanamgambo wa Boko Haram nchini humo kimewaachia huru wanafunzi wa kike 76.
Hawa ni kati ya 110 ambao walitekwa mwezi uliopita katika Mji wa Dapchi. wasichana hao wamerudishwa na Boko Haram asubuhi bila kuwepo vurugu.
Taarifa aliyoitoa Waziri huyo imeeleza kuwa kikundi hicho kimewarudisha wasichana hao pasipo kufanya vurugu na kuhakikisha hakuna yeyote aliyeumia au kopoteza maisha. hata hivyo taarifa hii haijaeleza kama kuna wasichana waliokufa.
HUKUMU KESI YA DAWA ZA KULEVYA: Kilichompata Masogange siku ya hukumu