Leo June 28, 2018 Watu 15 wameripotiwa kufariki na wengine 70 kujeruhiwa baada ya moto kuzuka na kuliunguza soko la Gikomba lililopo Nairobi nchini Kenya.
Moto huo ambao ulianza kuwaka mnamo majira ya saa 2 asubuhi leo umesababisha Wafanyabiashara waliokuwa wakifanya biashara katika soko hilo kupoteza mali zao ambapo mpaka sasa thamani yake bado haijatajwa.
Jeshi la Polisi nchini humo limesema kuwa bado linafanya uchunguzi kubaini chanzo cha moto huo ulioteketeza mali nyingi za Wafanyabiashara katitka soko hilo na kuunguza baadhi ya nyumba zilizopo jirani na soko hilo.
Aidha imeelezwa kuwa soko hilo sio mara ya kwanza kuwaka moto limekuwa likikukumbwa na kadhia hiyo mara kwa mara.
Good News: MILIONI 600 zimetengwa kwaajili ya ujenzi wa Chuo Kikuu cha Waalimu wa Sayansi