Baada ya April 3 2016 shirikisho la soka Tanzania TFF kupitia kwa makamu mwenyekiti wake Jerome Msemwa waliamua kutangaza kutoa adhabu kwa viongozi, wachezaji na timu za Ligi daraja la kwanza zilizokuwa zinahusishwa timu za Kundi C katika upangaji wa matokeo.
TFF baada ya kupitia upya adhabu ilizotoa April 3 2016 imeamua kumfutia adhabu golikipa wa Simba aliyekuwa kwa mkopo katika klabu ya Geita Gold Denis Richard ambaye awali alitangazwa kupewa adhabu ya kufungiwa miaka 10 kucheza soka na faini ya milioni 10 kutokana na kutuhumiwa kwa upangaji wa matokeo.
Denis Ricahard alipatikana na hatia baada ya kumuomba muamuzi ruhusa ya kwenda kujisaidia na kukaa muda mrefu bila kurudi, hivyo kwa mujibu wa makamu mwenyekiti wa kamati ya rufaa Revocatus Uhuri amemfutilia mbali adhabi hiyo na kusema refa ndio alishindwa kumudu mchezo.
Hata hivyo katika rufaa hiyo ni Denis Richard pekee aliyefutiwa adhabu, kama ulikosa waliopewa adhabu April 3 2016 Bonyeza HAPA
CHANZO : Salehjembe
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE
ALL GOALS: AZAM FC VS ESPERANCE (FULL TIME 2-1) APRIL 10 2016
https://youtu.be/duzv5kA8Q-c