Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa amewataka wananchi kutunza vyanzo vya maji ili viwe endelevu kwa vizazi vijavyo, sambamba na kuacha kuendesha shughuli za kilimo pembezoni mwa mito.
Profesa Mbarawa ameyasema hayo wakati wa kutekeleza Kampeni ya Upandaji Miti mwa mto Mzinga, ambapo amewataka wananchi kulinda vyanzo vya maji ili wapate majisafi na salama kwa manufaa yao na vizazi vijavyo.
“Lazima tusimamie sheria, serikali inawekeza hela nyingi sana katika kujenga miundo mbinu na kampeni hii imeanzia Mtwara, Ruvuma na Dar es salaam na hii itaendelea nchi nzima,”.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva amesema mtambo wa maji wa Mtoni Mtongani ulijengwa mwaka 1949 ambapo unahudumia mkoa mzima wa Dar es Salaam.
“Nilianza na nitaendelea kupanda miti pembezoni mwa vyanzo vya maji, suala hili nimeliwekea kipaumbele maji ni muhimu na wananchi wanahitaji maji,” amesema Lyaniva.