Jumanne ya April 26 2016 mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ndio ulichezwa, mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ulichezwa katika jiji la Manchester uwanja wa Etihad, huu ni mchezo ambao ulikuwa unazikutanisha Man City dhidi ya Real Madrid.
Huu ni mchezo ambao takwimu zilikuwa zinaibeba Real Madrid kwa kiasi kikubwa kuliko Man City ambao walikuwa nyumbani, 24 July 2015 Man City akiwa nyumbani alifungwa goli 4-1 na 21 Nov 2012 alitoa sare ya goli 1-1 katika uwanja huo wa Etihad, takwimu ambazo hazioneshi dalili nzuri akicheza na Real Madrid katika uwanja huo.
Licha ya kuwa mchezo umemalizika kwa sare ya 0-0, Real Madrid kwa mujibu wa takwimu walikuwa wanatajwa kuwa na safu imara ya ushambuliaji kuliko Man City , kwani Real katika mechi zake tano zilizopita hivi karibuni walikuwa wamefunga jumla ya magoli 18 na kufungwa matatu, wakati Man City walikuwa wamefunga magoli 11 na kufungwa mawili.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE
ALL GOALS: AZAM FC VS ESPERANCE APRIL 10 2016, FULL TIME 2-1
https://youtu.be/duzv5kA8Q-c