China ni nchi ambayo imekuwa ikitajwa kuwa na taratibu na Sheria ambazo zinabana sana kuzagaa kwa picha na video za ngono mitandaoni na hata kuuza mitaani, hata namna ambavyo wameweka ulinzi mkubwa kwenye system za mitandao, ni ngumu sana kwa mtu kusambaza picha au video hizo ndani ya China.
Majaji watatu Uingereza wamefukuzwa kazi baada ya kukutwa na hatia ya kutumia mtandao na Computer za ofisi ya Mahakama kuangalia video za ngono.
Msimamizi wa idara ya Mahakama amesema kuwa Majaji hao, Timothy Bowles, Warren Grant na Peter Bullock walitumia Computer za ofisi kuangalia video za ngono, ni kinyume na taratibu na maadili ya ofisi ya Umma.
Hivi mfano ikifanywa utafiti Bongo kuonesha watu ambao wako maofisini na wanaangalia hizi picha na video unadhani matokeo yake yatakuwaje mtu wangu? Nasubiri kuona utakachoniandikia.
Kwenye Facebook, Instagram na Twitter natumia jina la millard ayo mtu wangu, jiunge na mimi niwe nakusogezea kila taarifa inayonifikia, kujiunga na mimi bonyeza >>>twitter Insta Facebook