Watu 7 wamefariki na wengine 26 kujeruhiwa baada ya basi la Msanga Express lililokuwa linatokea Morogoro kwenda Mahenge kugongana na basi la Luwinzo lililotokea Njombe kwenda Dar katika eneo la mbuga ya Mikumi.
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi ambapo dereva wa basi la Msanga alikuwa akijaribu kulipita lori, basi hilo likagongwa upande wa kulia na kusababisha vifo vya watu sita hapo hapo na mwingine mmoja kufariki wakati akiwa anakimbizwa kupelekwa Hospitali.
Kamanda wa Polisi Morogoro, Leonard Paulo amesema mwili mmoja ndio uliotambulika na miili mingine 6 imehifadhiwa katika Hospitali ya St. Kizito Mikumi, madereva wa mabasi yote wamejeruhiwa na wanaendelea na matibabu chini ya ulinzi.
“Ilipofika hapa mvua ilikuwa inavyesha na kulikuwa na utelezi.. kilichotokea ni kwamba mbele kulikuwa na lori ambalo limetoroka kwenye eneo la tukio, kwa hiyo baada ya kuliona lori alitaka kulipita kwa upande wa kulia wakati analipita huyo mwenye basi kwa mbele ghafla kulikuwa na gari lingine”– Kamanda wa Polisi Morogoro, Leonard Paul.
Muunguzi wa zamu Katika Hospitali ya St. Kizito, Joseph Masenga amekiri kupokea majeruhi 26 na kusema kwa sasa wanaendelea vizuri na matibabu.
Ili kusikiliza taarifa hiyo iliyoripotiwa na kituo cha ITV bonyeza play hapa chini…
Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza>>> twitter Insta Facebook