Facebook, Twitter na Instagram imekuwa sehemu ya mitandao maarufu kwa watu kushare taarifa mbalimbali, lakini kutokana na mitandao hii kukua kwa kasi mara nyingi kumekuwa na mvutano juu ya sheria ambazo zinawekwa ili kudhibiti matumizi mabaya ya mitandao hiyo.
India walipitisha sheria ambayo tayari kuna watu wako kifungoni kutokana na kukiuka sheria hiyo, lakini leo kuna taarifa tofauti inayohusu ishu ya Mahakama Kuu India kufuta kipengele cha sheria kilichokuwa kikiamrisha mtu yoyote akiandika ujumbe wa kichochezi kwenye mtandao ashitakiwe.
Kulingana na kipengele hicho watu walioikashifu Serikali na idara zake India walikuwa wakikamatwa na kufungwa kifungo mpaka cha miaka mitatu.
Mwaka 2012 wasichana wawili walikamatwa Mumbai kwa kutoa maoni yao kufuatia mauaji ya mwanasiasa maarufu Bal Thackeray, mwingine alikamatwa kwa ishu ya kukashifu Serikali, lakini yupo aliyefungwa kutokana na ku’like” ujumbe huo.
Kumekuwa na idadi kubwa ya wanaharakati waliokamatwa kutokana na sheria hiyo ambayo mara zote imekuwa ikipingwa kwamba ni ya kikatili.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza>>> twitter Insta Facebook