Kutoka Mbagala Dar ndiko Hekaheka ya leo inapotokea ambayo inahusu mama aliyeolewa na kupewa zawadi ya kabati la nguo na somo wake, lakini baada ya muda mrefu kupita akaenda kwa bibi harusi huyo na kudai kabati lake kwa madai hana fadhila.
Mama huyo amesema somo yake alimpa zawadi ya kabati lakini badae alimtuhumu kuwa hana fadhila na hajawahi kumpa zawadi yoyote, akaamua kuchukua kabati lake kitendo kilichomkera mume wake wa mama huyo na kuamua kumnunulia mke wake dressing table mpya.
Basi wakaitwa marafiki, ndugu na majirani ili kushiriki sherehe ya kicheko ambayo mtangazaji wa Hekaheka Geah Habib alialikwa pia.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza>>>twitter Insta Facebook