Vyombo vya habari vimeripoti taarifa mbalimbali kuhusu Afya ya Askofu Josephat Gwajima ambae alikuwa amelazwa katika Hospitali ya TMJ toka siku ya Jumamosi baada ya kuanguka wakati akihojiwa na Polisi Makao Makuu DAR.
“Hali ya Afya yangu inaimarika naendelea vizuri sasa.. nasema viongozi wa dini lazima wawe wakweli jambo linaloamuliwa na viongozi wa dini lazima kiongozi wa dini aheshimu na amentain kile kilichokuwa kimesemwa na maaskofu” –Askofu Gwajima.
Daktari aliyekuwa akimhudumia Askofu huyo katika hospitali TMJ amesema kuwa Afya ya mgonjwa wake inaendelea vizuri; “Ni kweli kwamba tulikuwa tumemlaza Mchungaji Josephat Gwajima katika Hosptitali yetu kuanzia siku ya Ijumaa ya tarehe 27.. tulimlaza ICU na amekaa kule kule ICU kuanzia siku ya Ijumaa hadi Jumatatu alipopata nafuu kidogo tukamuondoa ICU, tukampeleka general ward ambapo ameendelea kutibiwa kutoka ile jana hadi Jumatatu mpaka leo Jumanne, tukaona hali yake ime improve kwa kiasi kikubwa na tukaona pamoja kwamba sio kwa asilimia mia moja, lakini anaweza kuruhusiwa kwenda nyumbani na anaweza kuendelea na matibabu akiwa nje.“–Dr. Fotrunatus Mazigo.
Kuhusu kuwa na walinzi Hospitalini hapo daktari amesema ni kweli alikuwa na walinzi.
Ili kusikiliza taarifa hiyo bonyeza play hapa chini, hii ilikuwa exclusive kwenye AMPLIFAYA jana MARCH 31.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza>>>twitter Insta Facebook