CIES Football Observatory imetoa orodha ya wachezaji bora katika vipengele vitano tofauti ambapo mastaa mbalimbali wametokea kwenye list hiyo.
Katika chati hiyo Gael Clichy wa Manchester City amefanikiwa kuwa beki bora wa kulia huku Mesut Ozil wa Arsenal akichaguliwa kama kiungo bora mshambuliaji sambamba na Eden Hazard wa Chelsea.
Kwa upande wa washambuliaji Lionel Messi mwenye mabao 19 amefanikiwa kushika nafasi ya kwanza kwa kupata pointi 100 akifatiwa na Arjen Robben mwenye 92 huku nafasi ya tatu ikishikwa na Bas Dost Wolfsburg mwenye pointi 72.
Cristiano Ronaldo ambaye amefunga mabao sita tangu ashinde tuzo ya Ballon d’Or iliyotolewa mwezi January anakamata nafasi ya 29.
Orodha ya washambuliaji 10 bora Ulaya na points walizopata
1. Lionel Messi, Barcelona (100)
2. Arjen Robben, Bayern Munich (92)
3. Bas Dost, Wolfsburg (77)
4. Luis Suarez, Barcelona (71)
5. Diego Costa, Chelsea (61)
=6. Harry Kane, Tottenham Hotspur (57)
=6. Marco Reus, Borussia Dortmund (57)
8. Lucas Barrios, Montpellier (56)
9. Pierre-Emerick Aubameyang, Borussia Dortmund (55)
10. Christophe Mandanne, Guingamp (54)
Viungo 10 bora washambuliaji
1. Eden Hazard, Chelsea (100)
=1. Mesut Ozil, Arsenal (100)
3. Jesus Navas, Man City (86)
4. Kevin de Bruyne, Wolfsburg (85)
5. Shinji Kagawa, Borussia Dortmund (84)
6. Marek Hamsik, Napoli (79)
7. David Silva, Man City (77)
8. Maximilian Meyer, Schalke (73)
=9. Roberto Pereyra, Juventus (72)
=9. Javier Pastore, PSG (72)
Mabeki 10 bora wa kati
1. Emir Spahic, Bayer Leverkusen (100)
2. Martin Demichelis, Man City (89)
3. Mats Hummels, Borussia Dortmund (79)
4. Chris Smalling, Man Utd (76)
5. Thiago Silva, PSG (71)
=6. David Luiz, PSG (69)
=6. Stefan de Vrij, Lazio (69)
8. Marcos Rojo, Man Utd (68)
=9. Konstantinos Manolas, Roma (64)
=9. Neven Subotic, Borussia Dortmund (64)
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook