Kwenye zilizoandikwa kurasa za Magazeti na kuchambuliwa kwenye Power Breakfast @CloudsFM leo April 03 2015 iko story ya NEC kutangaza kuahirishwa kura ya maoni ya katiba inayopendekezwa, CHADEMA wasafiri kwa ndege kutafuta majimbo kanda ya ziwa, Jeshi la Polisi limeshindwa kumhoji Askofu Gwajima kutokana na Afya yake, mama wa msichana anayedaiwa kutaka kujiunga na kundi la Al-Shabaab amesema anamuachia Mungu, iko pia stori ya wagonjwa kubebwa kwenye machela kilometa 10 kwenda Hospitali Mbeya.
Nyingine iliyoandikwa ni ishu ya watu 147 kuuawa Chuo kikuu cha Garissa Kenya katika shambulio la kigaidi, muswada wa Sheria ya makosa ya mtandao waibana Serikali, mgomo wa wafanyabiashara wamalizika rasmi baada ya Mwenyekiti wao kuachiliwa, Polisi kuimarisha ulinzi katika sikukuu za Pasaka, ACT imesema haina mpango wa kujiunga na UKAWA, kuna stori nyingine ya wadau kuukosoa muswada wa vyombo vya habari TZ.
100.5 Clouds FM inasikika ukiwa Nachingwea.
Iko hapa sauti yenye uchambuzi wote, bonyeza play kuisikiliza…
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook