Hekaheka ya leo April 13 ni mwendelezo wa ile iliyosikika April 8 kuhusu wanawake waliojipanga kumsuta mwenzao kutokana na maneno ya ugombanishi aliyokuwa akisambaza, wengine wakawa wanapiana kabisa yani.
Kama unakumbuka siku ambayo ilisikika sehemu ya kwanza ya Hekaheka hii huyo mwanamke alikimbia baada ya kufikishiwa story kwamba wenzake wanaenda kumsuta.
Baadae mwanamke huyo aliamua kuwafuata wanawake hao na kuwaomba msamaha.. katika kuomba msamaha akazusha maneno mengine na kuibua ugomvi mwingine upya.. akaoba msamaha kwa mara ya pili, kabla hajamaliza akatokea mwanamke mwingine aliyedai kuambiwa maneno mengine tena na mwanamke huyohuyo.
Ishu juu ya ishu, akaona hili balaa limekua kubwa, akaamua kukimbia.. hawakumuacha, nao wakaanza kumkimbiza huku wanamzomea japo hawakumkamata.
Sikiliza Hekaheka yote kwa kubonyeza play hapa chini…
millardayo.com ni sehemu yako utakapozipata zote unazozitaka, vichekesho, stori za siasa, muziki, michezo, movies, magazeti, video mpya na nyingine kubwa…. unaweza kujiunga na mimi Facebook, Twitter na Instagram pia zitakufikia zote mtu wangu, jiunge hapa >>>twitter Insta Facebook