Stori kubwa zilizosikika kwenye Magazeti ya leo April 17, kupitia show ya PowerBreakfast ya Clouds FM , zikichambuliwa na Paul James nakukaribisha mtu wangu…
Dereva aliyebeba watuhumiwa wanaodaiwa kuwa magaidi Kidatu asimulia tukio hilo, Mkuu wa Mkoa Mwanza Magesa Mulongo amesema taarifa za magaidi kuvamia Mkoa huo sio za kweli, Mtanzania abuni kifaa cha kufundishia bila mwalimu, Mkurugenzi wa TEHAMA, Ally Simba amesema sheria za usalama wa mitandao zilizowasilishwa Bungeni hivi karibuni zimetungwa kukidhi matakwa ya kimataifa.
Nyingine zilizosikika iko ya binti anaedaiwa kubakwa na Emmanuel Mbasha vipimo vimeonesha hakufanyiwa kitendo hicho, Mbunge William Ngeleja amejikuta kwenye wakati mgumu wakati akizungumza na wananchi wa jimbo lake, Waziri Samuel Sitta amemsimamisha kazi Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya reli Kapallo Kisamfu..
Kulikuwa na mazungumzo na Katibu Mkuu wa jukwaa la wahariri Nevile Meena ambae ametoa mawazo yake juu ya Muswada wa Sheria ya Makosa ya Mtandao wa mwaka 2015 uliopitishwa na Bunge hivi karibuni.
Bonyeza play hapa chini ili kusikiliza uchambuzi wa story zote…
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook