Kumekuwa na ripoti ya habari za ajali mfululizo za magari TZ.. watu wengi wamefariki na wengine kupata majeraha kutokana na ajali hizo.
Ripoti ya Jeshi la Polisi iliyotoka siku chache zilizopita ilionesha kuwa Mwezi April 2015 umeongoza kwa kuwa na ajali chache lakini idadi ya watu waliofariki ni kubwa zaidi tangu mwaka 2015 uanze.
Naibu Waziri na Mbunge wa Bumbuli, January Makamba ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter, kuhusu kile ambacho aliwahi kupendekeza kifanyike ili kumaliza tatizo la ajali hizo.
Ajali za barabarani hazipaswi kuonekana kama jambo la kawaida. Kusafiri kwa basi hakupaswi kulinganishwa na kujitoa muhanga. Nilipendekeza:
— January Makamba (@JMakamba) April 17, 2015
1.Kuwe na taasisi mpya ya “Highway Patrol” yenye magari ya kutosha na askari waadilifu. Traffic kuwa na vijiwe mahsusi barabarani haisaidii.
— January Makamba (@JMakamba) April 17, 2015
2.Magari ya abiria yawe na kifaa ambacho kinatoa mlio mkali ndani ya basi spidi inapozidi na kutuma automatic SMS kwenye namba Maalum polisi
— January Makamba (@JMakamba) April 17, 2015
3. Highway Police wawe wanazunguka barabarani kila wakati badala ya kuwa na geti tu au kijiwe cha kupumzika.
— January Makamba (@JMakamba) April 17, 2015
4. Iwapo ajali itapatikana kutokana na ubovu wa basi, leseni ya kampuni ya mabasi isimamishwe. Hii itawafanya wenye mabasi wawe makini.
— January Makamba (@JMakamba) April 17, 2015
5. Magari yanayoharibika barabarani hayapaswi kupaki highway siku tatu yanapaswa kupewa masaa matatu kutengenezwa au kuondolewa barabarani.
— January Makamba (@JMakamba) April 17, 2015
6. Mamlaka ya usimamizi wa Usalama Barabarani kati ya SUMATRA na Polisi yabainishwe wazi ili kuwe na uwajibikaji.
— January Makamba (@JMakamba) April 17, 2015
7. Huduma za dharura za uokoaji wakati wa ajali, ikiwemo uwepo wa helikopta, ni muhimu. Watu wengine hufa kwa kuvuja damu nyingi tu.
— January Makamba (@JMakamba) April 17, 2015
8. Ujenzi wa barabara, kwa maana ya upana wa barabara, mabega na madaraja na alama na ishara za barabarani ni muhimu ukawa wa viwango.
— January Makamba (@JMakamba) April 17, 2015
9. Anapokamatwa dereva anayeendesha kwa uzembe, leseni yake isimamishwe papo hapo. Akiwa amelewa asiruhusiwe kuendesha tena gari la abiria.
— January Makamba (@JMakamba) April 17, 2015
10. Ndani ya basi, au kwenye tiketi, kuwe na namba za simu za kupiga au kutuma ujumbe Polisi abiria wakiona uendeshaji wa dereva hauridhishi
— January Makamba (@JMakamba) April 17, 2015