JAMBO LEO
Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema misukosuko aliyoipata katika Uliongo wa siasa kwa muda wa mwaka mmoja uliopita umemfanya awe na ujasiri na moyo wa chuma.
Zitto amesema ujasiri wake ulianza mwaka 2007 wakati wa sakata la BUZWAGI japo hakuungwa mkono na Wabunge wengi lakini alifanya kila jitihada kuhakikisha Watanzania wanajua uovu wa viongozi wao.
Zitto amesema hatojibu madai anayozushiwa kwamba amejiunga ACT ili kuwaandalia njia viongozi wengine ambao wanataka kugombea Urais.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama hicho Anna Mghwira amesema ni jambo la kusikitisha kuona watu wanashindwa kusimama na hoja za kimaendeleo badala yake wanakaa kusikiliza uzushi.
NIPASHE
Mwalimu wa chekechea Mollen Calleb, aliyesimama mahakamani kwa kujifanya mzazi wa mtoto wa miaka miwili aliyejeruhiwa kwa kupigwa na mlezi wa shule ya chekechea ya Nelca Day, amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela kwa kosa la kuidanganya mahakama.
Mwalimu huyo anatuhumiwa kuidanganya mahakama na kusababisha kesi hiyo ya kujeruhi kufutwa bila mlalamikaji kuwepo katika Mahakama ya Mwanzo Ilemela, Mwanza, ilifuta kesi ya kujeruhiwa mwanafunzi, inayomkabili mlezi wa shule ya chekechea ya Nelca Day Care, Siwema Bujota anayedaiwa kumpiga mtoto huyo na kumjeruhi sehemu mbalimbali za mwili.
Bujota aliyekuwa na dhamana ya kulea watoto shuleni hapo, alimjeruhi mwanafunzi wa miaka miwili (jina limehifadhiwa), kwa kumchapa viboko kwa madai kuwa alijisaidia haja kubwa shuleni.
Baada ya kesi hiyo kufikishwa mahakamani, mwalimu wa shule hiyo, Calleb alikwenda mahakamani na kujitambulisha kwamba yeye ndiye mlalamikaji wa kesi hiyo na kuiomba mahakama kuifuta kwa madai kuwa hakuwa na nia ya kuendelea na mashitaka na kwamba watamalizana nje ya mahakama ambapo Mahakama hiyo ilifuta kesi bila kujua kwamba aliyesimama mahakamani sio mlalamikaji halali.
Mlalamkaji katika kesi hiyo alikuwa Sabrina Hamis, ambaye kabla ya kesi kuanza kusikilizwa alikwenda hospitali kwa matibabu ya mtoto huyo, ambaye hali yake ilibadilika ghafla akaamua kwenda kutoa taarifa kituo cha Polisi cha Kilumba, kulalamikia kesi yake kufutwa kinyemela.
Jeshi la polisi mkoani Mwanza lilianza kuwasaka watuhumiwa wote wawili akiwemo mshtakiwa na mwalimu aliyejifanya mlalamikaji.
Kaimu Kamanda, Kamishina Msaidizi wa Polisi Mwanza (ACP), Japhet Lusingu alisema kuwa Aprili 13 mwaka huu watuhumiwa hao walikamatwa na kufikishwa Mahakamani, baadaye akapata taarifa kwamba mwalimu huyo amefungwa miezi sita kwa kuidanganya mahakama.
MTANZANIA
Watu 38 wameripotiwa kufariki jana katika matukio mawili tofauti Mbeya na Shinyanga, ambapo tukio la Mbeya limetokea Tukuyu, gari ndogo aina ya Toyota Hiace ilitumbukia mtoni na baada ya kushindwa kukata kona wakati likiwa kwenye mwendokasi na tukio ambalo RPC wa Mbeya, Ahmed Msangi alithibisha kutokea ambapo watu 19 walifariki.
Kamanda Msangi amesema uchunguzi unaonesha gari hiyo ilipata ajali wakati ikikimbizwa na madereva wa Coaster ambao waliiona ikipakia abiria kitu ambacho madereva hao wa Coaster walikuwa wakipinga kwa kuwa walikuwa kwenye mgomo kutokana na dereva mwenzao kupigwa faini ya 250,000/=
Katika tukio jingine Kamanda wa Polisi Shinyanga Justus Kamugisha amethibisha kutokea tukio la watu 19 wanahofiwa kufariki kwa kufukiwa na kifusi cha udongo katika machimbo madogo ya dhahabu kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha Mkoa huo.
Diwani wa Kata ya Lunguya ambako limetokea tukio hilo amesema huenda idadi ya watu waliofukiwa ikawa kubwa zaidi kutokana na eneo ambalo kifusi kimejifukia kuna watu wengi waliokuwa wakiingia kuchimba dhahabu.
“Nimeshatuma kikosi cha Polisi kwenda kusaidia kuokoa, lakini idadi ya watu waliokufa tumeambiwa ni kuwa ni 19.. hatuna uhakika nayo..”—Kamanda Kamugisha.
MTANZANIA
Licha ya Rais Jacob Zuma kulaani vurugu zinazoendelea Afrika Kusini dhidi ya wageni vurugu hizo zimezidi kupamba moto na kuvuka mipaka ya nchi hiyo,
Raia wa Afrika Kusini wanaoishi nakufanya biashara katika nchi za Msumbiji na Zimbabwe nao wameanza kushambuliwa ambapo malori yenye namba za usajili za Afrika Kusini yameshambuliwa Msumbiji, huku wanafunzi wa Vyuo vikuu Zimbabwe nao wakiandamana na kufanya fujo kwa wafanyabiashara na wawekezaji waliopo nchini humo.
Balozi wa Tanzania aliyeko Afrika Kusini amesema kuwa hakuna Mtanzania aliyeshambuliwa wala kuathirika na vurugu hizo.
Mmoja wa Watanzania ambao wanaishi karibu na mpaka wa Afrika Kusini na Msumbiji amesema malori zaidi ya 100 yanayosafirisha makaa ya mawe yamekwama baada ya mpaka kufungwa.
MTANZANIA
Askofu Gwajima ameshitakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu pamoja na wenzake watatu kwa makosa mawili ya kutoa lugha ya matusi na uzembe wa kuhifadhi silaha yake ya moto ambayo anaimiliki kihalali.
Askofu huyo amesomewa mashtaka ya kutoa lugha ya matusi kwa Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Kardinali Polycarp Pengo, lakini Askofu Gwajima alikana mashtaka yote mawili na kuachiwa kwa dhamana mpaka Mei 4 mwaka huu.
Kabla Askofu huyo hajafikishwa Mahakamani nyumba yake ilizingirwa na Askari Polisi kwa muda wa saa nane toka saa 12 asubuhi, milango ya nyumba hiyo ilikuwa imefungwa huku waumini waliokusanyika nje ya nyumba hiyo pia wakiwashutumu Polisi kwa kumng’ang’ania baba yao wa kiroho.
Ilipofika majira ya saa 6:03 walifika baadhi ya viongozi wa Kanisa la Ufufuo na uzima pamoja na Mwanasheria wa Askofu huyo na kufanya kikao kidogo na Askari Polisi hao ambapo baadae waliondoka kuelekea Centre Police wakiwa na Askofu huyo, ambako haikuchukua muda akatolewa na kupandishwa Mahakama ya Kisutu.
MWANANCHI
Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Francis Isack amewasweka ndani watendaji 16 wa vijiji na kata kwa madai ya kuzembea kusimamia maabara za Sekondari ambapo mwenyewe amesema hiyo ni hatua ya kukumbushana majukumu kwa kuwa wao ni Watendaji wa Serikali ambao hawakupaswa kuzembea.
Mkuu huyo wa Wilaya amesema hatua hiyo ni ya kukumbushana majukumu yao waliyopewa na Serikali.
Amesema baada kuwahoji walitoa majibu mepesi kwamba wamezuiwa na madiwani kukusanya michango kwa wananchi.
millardayo.com ndio sehemu yako kuzipata story zote mtu wangu, unaweza kuwa karibu zaidi na mimi kwa kujiunga kwenye Facebook, Twitter na Instagram pia zitakufikia zote mtu wangu, jiunge hapa >>>twitter Insta Facebook