Raia wa kigeni waliokuwepo Afrika Kusini wengi wao wamejikuta wakilazimika kurudi kwenye nchi zao bila kupenda, hawakuwa na amani kutokana na machafuko ambayo yalitokea na kusababisha wengine saba kuuawa.
Akiongea kwenye habari ya Clouds FM Mtanzania ambaye ameishi South Africa kwa miaka 7 Calvin Nyamori amesema sio mara ya kwanza kwa wageni kukumbana na mashambulizi ya aina hiyo; >>“ Ishu ya Xenophobia ni ishu ya kitaifa South Afrika kwa sababu sio mara ya kwanza safari hii imekuwa kubwa zaidi safari hii imewashinda mpaka jana Rais Jacob Zuma kasema jeshi liingie mzigoni, kwa hiyo ni kama unavyoona Chief wa Wazulu anatekeleza maagizo ya Zuma kwa maana kwamba katika kipindi cha kampeni wakati Jacob Zuma anaingia madarakani haya ndio maagizo aliyopewa na Wazulu, kwamba watu ambao sio wenyeji lazima warudi kwao sasa wameshindwa kuitekeleza rasmi matokeo yake wanatumia makundi mengine kama Machifu na watu wengine ili hao watu wengine waweze kuondoka >>>amesema Calvin Nyamori.
>>Tumeathirika mpaka sasa hivi ni watu 4 wamethibitika wamekufa>>> Calvin Nyamori.
Katika taarifa ambayo ilitolewa na Waziri Membe alisema kuwa hakuna Mtanzania yoyote aliyepoteza maisha kutokana na mashambulizi hayo.
Ili kusikiliza taarifa hiyo iliyoripotiwa na kituo cha Clouds FM bonyeza play hapa chini…
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenyeTwitter,Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa>>>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.