Mwaka 2007 huko India kulitokea habari yakushangaza kidogo baada ya ndama kunaswa akimla kuku na kuleta sintofahamu miongoni mwa wakazi.
Hii tena imetokea huko Kenya na kukaa kwenye headlines baada ya mkulima mmoja kusema kuwa mmoja wa ng’ombe wake anaowamiliki amesusia lishe yake ya kawaida anayopewa kila siku na kuanza kuwala kondoo wake.
Mkulima huyo Charles Mamboleo, ambaye anamiliki shamba Kusini Magharibi mwa Nakuru aligundua kuwa ng’ombe wake amemla kondo siku moja asubuhi wakati akimpa chakula lakini jitihada zake za kumpa ng’ombe huyo chakula na maji hazikufua dafu, na siku iliyofuata ng’ombe huyo alimla kondoo mwingine.
Kulingana na afisa mmoja wa kilimo alisema huenda tabia ya ng’ombe huyo imetokana na ukosefu wa madini yanayopatikana kwa mimea mibichi.
Hakuna Stori itakayokupita mtu wangu,niko tayari kukutumia wakati wowote kupitiatwitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook