Imetokea Kibaha kwenye mkoa wa Pwani Tanzania, ilitangazwa kwamba Marehemu kazikwa na vitu vya thamani ambavyo akiwa hai alisema angependa azikwe navyo, maziko yakafanyika salama akazikwa na sanduku lake.
Baada tu ya kuzikwa kuna mlinzi alipewa kazi ya kulinda kaburi mpaka likauke ambapo baada ya kulinda kwa zile siku walizokubaliana, siku ya kwanza baada ya siku za mlinzi kumalizika Wezi wakaja kulifukua kaburi kama inavyoonekana hapo juu na wakaiba sanduku, wakamvua Marehemu soksi na inasemekana walitaka kumvua na nguo zake pia ikashindikana.
Hizi ni picha ambazo nimekusogezea hapa.. ndugu waliamua kulijenga upya baada ya wezi hao kubomoa na kuiba vilivyokuwemo ndani.
Shuhuda anasema hata hivyo baada ya kaburi kubomolewa na wezi, mtu mmoja ambaye alikua akikata majani maeneo ya karibu na makaburi alisema ameona nguo zilizotawanywa kutoka kwenye sanduku na ikajulikana ndizo alizozikwa nazo Marehemu, zikakusanywa na kuchomwa moto.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limethibitisha tukio hilo, linawatafuta waliovunja kaburi hilo na kufanya uhalifu wa kuiba nguo na vitu vingine alivyozikwa navyo.
Unaweza kuisikiliza stori kamili kwenye sauti hapa chini.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa>>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribeYouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.