Dunia imekuwa na mengi ambayo yanahusiana na Teknolojia.. kila siku kuna story mpya, moja ya zilizowahi kuchukua headlines mwaka 2014 ilikuwa ni ishu ya magari ambayo yanajiendesha yenyewe bila dereva.
Google pamoja na makampuni mengine yaliamua kuweka nguvu kwenye ubunifu huu, naambiwa mwezi September 2014 California Marekani iliruhusu magari hayo yaendelee kutembezwa katika barabara za kawaida ambazo zinatumiwa na magari mengine pamoja na watu.
Ripoti iliyotoka leo May 11 2015 inaonesha kuwa katika magari 50 ambayo yanatembea bila dereva California, zimewahi kutokea ajali nne tu ambazo zinahusisha gari hizo.. japo Google wanasema ajali ambazo zilitokea ni ajali ndogo tu za kawaida.
Ripoti hii ni kama inatia ushawishi wa nchi nyingine kuvutiwa na huu ubunifu na kuanza kutumia aina hii ya magari.. kingine kilichopo njiani ni hili lori ambalo nalo liko njiani kuja, nalo linatembea bila dereva.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyezahapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.