Nchi nyingi duniani zimekuwa zikikabiliana na matumizi ya bidhaa feki ikiwemo vyakula na vipodozi ambavyo kwa kiasi kikubwa huathiri afya za watumiaji.
Huko Uingereza imeelezwa kuwa kinyesi cha panya na mkojo ni baadhi ya viungo vinavyotumika kutengeneza bidhaa feki za urembo kwa wanawake.
Utafiti wa bidhaa za urembo zikiwemo mafuta ya kujipaka na marashi zinazouzwa kwa njia ya mtandao nchini Uingereza imebainika zinatengezwa kwa njia isiyofata sahihi kwa kushindwa kulinda afya za binadamu
Polisi waliofanya uchunguzi huo, wamedai mfumuko wa bei ya bidhaa kwa njia za kielektroniki umechangia ongezeko la mauzo ya bidhaa hizo.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.