May 20 2015 tayari Magazeti yako mtaani, labda umejua machache ambayo yameandikwa mengine bado hayajakufikia.
Hapa nimekurekodia uchambuzi wa stori za Magazetini uliofanyika redioni, kwenye stori kubwa iko ya Ripoti ya CAG kuhusu ufisadi wa Mabilioni kwenye taasisi mbaimbali za Serikali TZ.. nyingine inahusu hali mbaya ya kiafya kwa wakimbizi wa Burundi waliopo Kigoma TZ, 20 wamefariki mpaka sasa kwa ugonjwa wa kuhara.
Kingine ni stori ya hali ya machafuko ambayo inaendelea Burundi, TZ imetwaa Tuzo ya kuwa kinara kwenye Utalii, Kikao cha madereva na Serikali bado ngoma nzito, Kiongozi wa CHADEMA atiwa mbaroni.. kuna stori pia kuhusu wafanyakazi wa Kiwanda cha Sukari Mtibwa wameandamana wakidai malimbikizo ya mishahara yao.
Wachinjaji wa ng’ombe Dar wameamua kuchinjia porini baada ya machinjio za Dar kufungwa, kuna stori pia inayohusu viongozi wastaafu waliosema TZ kwa sasa kuna viashiria vingi vya uvunjifu wa amani.
Ukiplay hapa utasikia pia alichokisema mtaalamu wa Uchumi pamoja na mtafiti wa Sera za Uchumi kuhusu ufisadi uliofanywa TZ.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.