Jana ilikuwa headlines za mgomo wa wanafunzi Chuo Kikuu Dar, leo imesikika ishu ya kutaka kuibuka mgomo na maandamano Iringa na Polisi wakaingilia kati.
Hii leo ilikuwa Bungeni Dodoma, swali kutoka kwa Mbunge Esther Bulaya; >>“Jana wanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam wamegoma sababu hawakupelekewa fedha za kujikimu.. wanafunzi wengi wanatoka maeneo ya vijijini watoto wa maskini, Chuo Kikuu cha Saint Joseph wameamua kuwarudisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza kwa sababu ya kukosa fedha.. Tunahitaji majibu ya Serikali kwa nini hawapeleki fedha za kujikimu kwa wanafunzi mpaka wanafunzi wagome?”>>
Majibu ya Naibu Waziri Mwigulu Nchemba >> “Niwaombe radhi wanafunzi wa vyuo vikuu.. Tuliongea na viongozi wa vyuo pamoja na bodi na Wizara inayosimamia, kulikuwepo na utaratibu wa kuipa fedha hizo na mpaka jana tayari fedha ilishatoka Wizara ya fedha.. wataalamu ambao wanashughulikia kuzifikisha hizo fedha kwa wanafunzi watoe kwanzaq fedha hizo ndio wakae vikao kuliko kusubiri kupitisha kwa utaratibu ambao wanafunzi wataendelea kupata shida”>>
>>“Serikali tunajitahidi kuhakikisha kwamba tunawafikishia kwa wakati fedha.. Serikali imeshatoa fedha na taasisi zinakopita wajitahidi leo leo vyuo vyote viwe vimeshapata fedha hizo”>> Naibu Waziri Mwigulu Nchemba.
Maswali na majibu kutoka kwa Mbunge Esther Bulaya na Naibu Waziri Mwigulu Nchemba uaweza kuisikiliza hapa kwa kuplay sauti.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.