Mei 21 Tanzania tuna kumbukumbu ambayo sio rahisi kufutika, kumbukumbu hii ni ajali ya kuzama kwa meli ya Mv Bukoba mwaka 1996, watu wengi walifariki kwenye ajali hiyo.
Mwanamitindo Flaviana Matata ni miongoni mwa watu ambao walipoteza watu wao wa karibu, yeye alimpoteza mama yake mzazi kwenye ajali hiyo, kila inapofika tarehe na mwezi huu kuna vingi anavyokumbuka.
Kwenye alichokisema kuna hii nukuu>>”May 21 ni siku ngumu sana kwangu na inazidi kuwa ngumu kadri siku zinavoenda.. nilimpoteza mama yangu, lakini kikubwa tulipoteza mamia ya Watanzania. Kinachotakiwa kuendelea ni kuwaombea hawa ndugu zetu waliotangulia.. Serikali na wanaosimamia usafiri wa majini wahakikishe jambo kama hili halitokei tena na kuzingatia usalama“>>
>>”Kila mwaka mimi ninakuja Mwanza naungana na Watanzania wenye mapenzi mema waliopoteza ndugu jamaa na marafiki kwa ajili ya ibada ya kumbukumbu ya ndugu zetu“>>
>>”Haukuwa msiba mdogo kwa hiyo kuiacha inapita hivi hivi sio vizuri.. natamani sana viongozi pia wangekuwa wanaona ukubwa wa siku hii.. leo kuna ibada alafu tutaelekea makaburini kwa ajili ya sala fupi”>> Flaviana Matata.
Unaweza kubonyeza play hapo chini mtu wangu kumsikiliza Flaviana Matata wakati anazungumza kwenye kipindi cha Power Breakfast kutoka Clouds FM.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.