Mwaka 1993 nchi ya Ireland ilikuwa moja ya mwisho mwisho kabisa katika nchi za Ulaya kuhalalisha ishu ya uhusiano wa jinsia moja.. mpaka leo ni miaka 22 imepita, wakati wowote huenda kukatokea headline nyingine kuhusu suala hilo, Bunge liliamua hii ishu washirikishwe watu wao pia na mpaka kesho Jumamosi May 23 2015 tutasikia nini kimepitishwa.
Watu wa Ireland wanaendelea kupiga kura leo, kama kura nyingi zikisema YES, basi Katiba ya nchi hiyo itafanyiwa mabadiliko na ishu ya ndoa za watu wenye uhusiano wa jinsia moja zitakuwa zimeruhusiwa rasmi kwenye nchi hiyo !!
Kuna vitu vingi vinaendelea Ulaya, Marekani na nchi nyingine ikiwemo hii ya kuhalalisha ndoa na uhusiano wa jinsia moja, kwa Afrika ni nchi chache zimetoa msimamo.. Uganda ni moja ya nchi ambazo zilikataa kuhalalisha ndoa za aina hiyo.
Kampeni zimeendelea mtaani, migahawani kuna mabango yaliyoandikwa “YES EQUALITY” kuonesha watu kwamba wapo watu ambao wako tayari kuyakubali mabadiliko hayo.
Mpaka sasa hivi ni nchi 19 duniani ambazo zimehalalisha ndoa za jinsia moja, kama majibu ya kura hizo za Ireland yataonesha watu wengi wamekubali basi jumla ya nchi zitakuwa 20.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.