Tumezishuhudia ajali nyingi TZ, watu wetu wengi wamefariki kwenye ajali hizo, wengine wamepata majeraha makubwa.. mara nyingi watu wamekuwa wakilaumu kwamba mwendo wa kasi unachangia ajali hizo, stori kutoka Bungeni Dodoma.. swali la Mbunge Prof. Peter Msolwa na liko jibu la Naibu Waziri Pereira Silima.
Swali>> “Vyanzo vikuu vya ajali za barabarani ni pamoja na mwendo mkali na ulevi wa madereva.. Serikali imefikia wapi katika zoezi la kufunga vidhibiti mwendo ili kupunguza ajali?>>
Kuhusu ulevi katika nchi nyingine kuna namna ya kumchunguza dereva kama amezidisha pombe kwa kutumia breathalyzer, je Serikali inatumiaje utaratibu huu ambao kwenye nchi nyingine umeonesha mafanikio”>>Mbunge Prof. Peter Msolwa.
Jibu>> “Mpango wa speed governor ulifaa mwanzoni lakini ukawa hauna maana.. sasa hivi tunahakikisha kwamba tutaweka car tracking system na pia tunatumia camera ya kupima mwendokasi>>
Kuna patrols ambazo zinafanyika kuona kama madereva wanafuata taratibu za mwendo ambazo zimeoneshwa kwenye barabara.. Kweli ulevi unasababisha mambo mengi na haikukosewa kuitwa baba wa maafa, hili ni tatizo kubwa>> Naibu Waziri Pereira Silima.
“Kwa sasa tunachofanya kabla dereva hajaanza safari tunatumia vipima ulevi ambavyo tukiona ana dalili ya kuwa ameongeza chochote haruhusiwi kuendesha basi.. kama tunamkuta katikati ya barabara amelewa adhabu tunayompa tunamnyang’anya leseni asiwe dereva wa gari ya abiria pengine anaweza kuendesha familia yake”>>—Naibu Waziri Pereira Silima.
Niliirekodi hii toka Bungeni, swali na jibu la Waziri utasikiliza hapa ukibonyeza play.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.