Inawezekana kuonekana ni kichekesho lakini ni kweli imetokea baada ya bibi Louise Bonito kujikuta anaangua kilio katika sherehe ya siku yake ya kuzaliwa huko Australia.
Bonito ambaye ni bibi wa miaka 102 anayeishi katika mji wa North Haven alijikuta akipoteza meno yake yote ya mbele wakati alipokuwa akizima mishumaa iliyokuwa juu ya keki aliyoandaliwa na familia yake.
Akiwa katika harakati za kupuliza mishumaa alishngaa kuona meno yake ya mbele yakidondoka na kubaki kibogoyo.
Baada ya tukio hilo ilimlazimu kuacha zoezi hilo na kuanza kulia jambo lililowahuzunisha wanafamilia, lakini wengine walikuwa wakiangua vicheko kutokana na tukio hilo.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.