Unapozungumzia kifo hakuna mwanadamu yeyote duniani ambaye atapenda kusikia ama kutaka kujua atakufa lini na ni kawaida kila mmoja huwa anaogopa anaposikia taarifa zinazohusiana na kifo.
Lakini kwa mzee Muhashta Murasi ambaye alikuwa fundi viatu aliyestaafu kazi hiyo mwaka 1953 akiwa na umri wa miaka 122, amesema anakisubiri kifo kwa hamu kubwa sana kwani amechoka kuishi.
Kwa sasa ana umri wa miaka 180 na alizaliwa mwaka 1835 na tayari ameingia kwenye kitabu cha dunia cha kumbukumbu cha Guines kwa kuwa ndiye binadamuu pekee mwenye umri mkubwa kuliko wote.
Alizaliwa katika mji wa Bangalore, India na kwa mujibu wa daktari aliyekuwa akimfanyia vipimo amedhibitisha kuwa amekua hana magonjwa ya mara kwa mara hali inayochangia kuendelea kuishi kwa muda mrefu.
Lakini mtandao wa World News Report umesema huenda habari za mzee huyo hazina ukweli wowote.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.