Matukio ya unyanyasaji kwa watoto yameendelea kuchukua headlines kila kukicha sehemu mbalimbali duniani.
Miongoni mwa matukio yaliyosikika siku za hivi karibuni ni pamoja na lile la mfanyakazi wa ndani kumtesa mtoto kule Uganda, na kule India kuna lile la mtoto wa siku nne kulazimishwa kutembea na mganga kwa madai atapona..Yote haya ni matukio ya unyanyasaji kwa watoto.
Hili lingine limetokea hujo Ufilipono baada ya mama kuamua kumfunga mtoto wake mnyoyoro na kumwekea chakula kama mbwa kwa madai amekua akimsumbua.
Mama huyo aliweka picha za mwanaye huyo wa kiume akiwa uchi kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook, lakini picha hizo zilichukuliwa na wanaharakati wa haki za binadamu na kumfungulia mama yake mashtaka.
Mmoja wa wanaharakati hao Lurleen Hilliard. alisema kwa sasa mtoto huyo atakua chini ya kituo cha kulelea watoto wakati mama yake akitumia adhabu kwa unyanyasaji alioufanya.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.