Utapeli ni ishu ambayo iko sana mjini.. wakati mwingine unatapeliwa na mtu ambae hata hukutarajia, jamaa mmoja ambae anafanya biashara ya kuuza magari ametapeliwa na mtu ambae ni mlemavu Dar.
Kukutana kwao ilitokana na dalali mmoja ambae aliwaunganisha ili wauziane gari, baadae wakaenda Benki Kariakoo ambako alidai kwamba alitumiwa pesa na wafadhili wake walioko nje ya nchi.
Ikashindikana kutoa pesa kwa sababu alikuwa hana account ya dola, ikawa kunatakiwa pesa ili taratibu za kufungua account zikamilike.. huyo jamaa akatoa pesa hizo pamoja na pesa nyingine nyingi kumhudumia hoteli na vitu vingine wakati wanasubiri account hiyo ifunguliwe.
Story ni ndefu, timu ya #LeoTena wamesema hii Hekaheka itaendelea kesho ili tusikie jinsi utapeli ulivyofanyika.. iliyosikika leo sehemu ya kwanza unaweza kuisikiliza hapa.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.