Labda ishu ya kufua taulo hauizingatii sana kwa vile unalitumia tu mara moja alafu unalitundika mpaka baadae au kesho.. hivi una mpangilio maalum wa siku za kufua taulo lako, au huwa unalifua baada ya kulitumia mara ngapi?
Wataalamu wana hiki walichokishauri, wamesema unatakiwa kulifua taulo hilo baada ya kulitumia mara tatu au mara nne tu na sio zaidi ya hapo !!
Wanasema kama ukizidisha hapo kuna uwezekano mkubwa wa taulo kuzalisha bacteria ambao wanaweza kukuletea matatizo mengine kwenye ngozi.
Kingine kinachoshauriwa ni hiki, unaambia ni vizuri uwe unaning’iniza taulo sehemu ambayo linaweza kukauka kwa urahisi zaidi na usilichanganye na nguo au kitu kingine chochote kitakachofanya lichelewe kukauka.
Una comment yako hapo? Unaweza kuniandikia mtu wangu nione wewe uko upande upi !!
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.