Kuna ishu ya jinsia ya mtoto anaezaliwa, kati ya wazazi huenda ikatokea kati yao akawepo mmoja ambae anatamani kuwa na mtoto wa kike na mwingine akawa anatamani awe na mtoto wa kiume..
Rameshwar Rao aliamua kumfungia mkewe na mtoto wake wa kike bafuni kwa muda wa miaka mitatu kisa tu mwanamke huyo amejifungua mtoto wa kike wakati mwanaume alikuwa anahitaji kuwa na mtoto wa kiume.
Baada ya mkewe Priyanka kugundua ni mjamzito wa mtoto wa kike alimwambia mumewe ambaye alimtaka aitoe mimba kwa kuwa alitaka mtoto wa kiume, lakini mkewe alikataa kuitoa na kuamua kurudi kwa wazazi wake akajifungue.
Mwanamke huyo alitaka kukimbia baada ya kujifungua, mwanaume akaamua kumkamata na kumfungia kwenye choo pamoja na mtoto wao wa kike kwa muda wa miaka mitatu huku akiwa anawapa wali na maji kwenye bakuli kila siku.
Kwa sasa mwanaume huyo anashikiliwa na polisi baada ya marafiki wa familia yake kugundua kitendo alichokifanya kwa mkewe lakini mke wake amewaomba polisi hao kumwachia huru ili waendelee kuishi pamoja.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.