Kwa takribani wiki mbili sasa neno ‘rushwa’ limekuwa likiliandama sana shirikisho la soka duniani FIFA.
Wiki iliyopita maafisa 10 wa shirikisho hilo walikamatwa na serikali ya Marekani kwa kujihusisha na skendo ya ubadhirifu wa £100m, jambo ambalo lilipelekea wadau mbalimbali kumuomba Rais wa shirikisho hilo Sepp Blatter kujiuzulu.
Hata hivyo Blatter amegoma kufanya hivyo, lakini ikiwa suala la ubadhirifu wa £100m likiwa bado la moto, leo hii umetolewa ushahidi kwamba katibu mkuu wa FiFA Jerome Valcke alihusika na rushwa ya $10m kutoka kwa shirikisho la soka la Afrika ya kusini.
Kwa mujibu wa mkuu wa shirikisho la soka la SA, Danny Jordaan, amethibitisha kwamb ni kweli nchi hiyo ililipa kiasi hicho kwenda Raisi wa shirikisho la soka la CONCACAF wa wakati huo, Jack Warner mnamo mwaka 2008, kwa jili ya kusaidia maendeleo ya soka barani humo na sio rushwa iliyosaidia nchi hiyo kupata uenyeji wa kombe la dunia mwaka 2010.
Kwa upande wa FIFA wamemtaja, muargentina Julio Grondona ndio alikuwa mhusika mkuu ktika kuidhinisha malipo hayo ya $10 million.
Grondona alikuwa na cheo cha umakamu wa raisi na pia mwenyekiti wa kamati ya masuala ya fedha ya shirikisho hilo, hata hivyo Grondona alifariki dunia mwaka 2014.
Kauli ya FIFA kwamba Grondona ndio alitoa ruhusa ya kufanyika kwa malipo hayo ya rushwa inaonekana kumsafisha Jerome Valcke, baada ya gazeti la New York Times kutoa taarifa kwamba Valcke ndio aliyeidhinisha malipo hayo ya rushwa.
Lakini leo hii umetolewa ushahidi wa barua unaonyesha Valcke ndio aliyeidhinisha malipo hayo ikiwa ni rushwa kutoka nchi ya South Africa ambayo ilipewa uenyeji wa mashindano ya kombe la dunia mwaka 2010.
Mwendesha mashtaka wa Marekani amesema kwamba South African ililipa fedha hizo kwa Mr. Warner – ambaye wakati huo alikuwa makamu wa raisi wa FIFA ili kutimiza ahadi yao baada ya kupewa haki ya kuandaa kombe la dunia 2010.
Fifa iliichagua South Africa kuandaa fainali hizo mbele ya Morocco.