Licha ya kifungo cha mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius kuwa miaka mitano tangu alipohukumiwa mwakja jana, kuna taarifa huenda adhabu hiyo ikapunguzwa.
Mwanariadha huyo ambaye ni mlemavu alipatikana na hatia ya mauaji ya aliyekuwa mpenzi wake Reeva Steenkamp mwaka jana na huenda akasamehewa na kuaachiwa huru mwezi Agosti.
Mmoja wa viongozi wa idara ya masahihisho katika mahakama hiyo Zach Modise alisema uongozi uliokuwa ukisimamia kesi hiyo ulifikia maauzi hayo wiki iliyopita.
Kiongozi wa Mashtaka amekata rufaa ya kuachiliwa kwake na mahakama kuu ya rufaa itaanza kusikiza kesi hiyo mwezi Novemba na ataruhusiwa kutoka huku akiendelea na kifungo cha nje chini ya uangalizi maalum.
Maamuzi hayo yameonekana kuishtua familia ya Reeva Steenkamp na kudai kifungo hicho hakitoshi kuwa adhabu kwa kosa alilotenda.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.