Asamoah Gyan ni mmoja wa wachezaji wanaolipwa vizuri kutoka katika bara la Afrika, na hakuna uthibitisho mzuri wa kuonyesha ukubwa malipo yake zaidi ya ili hii mali mpya alionunua, jumba kubwa la kifahari.
Mshambuliaji wa Klabu ya Al Ain ambaye analipwa kiasi cha $200,000 kwa wiki amenunua jumba hilo lenye thamani inayokadiriwa kufikia dola millioni 3 za kimarekani ambazo zinafikia billioni 6 za kitanzania.
Jumba hilo lipo maeneo ya McCarthy Hills enclave jijini Accra lina baa mbili, bwawa kubwa la kuogelea. Lina ghorofa tatu zilizotengenezwa kwa muundo wa kipekee kila mmoja huku vifaa vya ulinzi vikiwa vya kisasa ikiwepo milango na madirisha yenye bullet proof.
Kwa mujibu taarifa za vyombo vya habari vya Ghana, Gyan aliinunua nyumba hiyo aliyoikarabati alipozuru nchini humo mwezi April wakati alipoenda kutazama pambano la masumbwi kati Emmanuel Tagoe na Jobert Delos Reyes.