Watu wengine wameanza kusahau kabisa headlines za #PanyaRoad.. nakumbuka iliwahi kuwa ishu kubwa sana January 2015, wapo waliopata majeraha wengine waliibiwa.. watu walizuka wakasema Panya Road wanavamia watu mitaani na kuwapiga wengine wanaiba !! Baadae hali ya hewa ikatulia.
Leo Mbunge Rachel Mashishanga akaibuka na mjadala kwamba ili kumaliza kabisa tatizo la Panya Road inatakiwa warudishwe Shule wote; “Hawa Panya road ukiwaangalia umri wao wanatakiwa wawepo Shule, Serikali ina mpango gani kuhakikisha inawakusanya vijana hawa na kuwapeleka Shule ili shughuli za uhalifu zipungue?”>>>– Rachel Mashishanga.
Hili ndio jibu la Naibu Waziri wa Fedha; “Kama nimekuelewa ni kwamba umesema tuwatafute wale Panya Road tuwakusanye alafu tuwapeleke Shule.. Sidhani kama tukisema Panya Road wote kusanyikeni hapa watasogea !! Tukubaliane kwamba kujiita Panya Road ni kosa, tusiwatukuze kwa jambo wanalolifanya“>>> Adam Malima.
“Tukubaliane kwamba wanachokifanya ni kinyume cha Sheria.. Tuwahamasishe vijana kwamba ziko njia mbadala badala ya hii ya kuwapora watu mali zao“>>> Naibu Waziri Adam Malima.
Hio story unaweza kuisikiliza kwenye hii sauti hapa mtu wangu.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.