Shambulio la Kigaidi limetokea Chad Jumatatu June 15 2015 katika Jiji la N’Djamena, watu 23 wakauawana wengine zaidiya 100 wakapata majeraha makubwa.
Waziri Mkuu wa Chad, Kalzeube Pahimi Deubet amesema mtu aliyelipua mabomu hayo alitumia vazi ambalo linavaliwa na wanawake wa kiislamu ambalo linaziba mpaka usoni… Kingine kilichoamliwa leo ni ishu ya kupigwa MARUFUKU kwa mtu yoyote kuvaa vazi hilo kwa mtu yoyote.
Agizo lililotolewa leo June 18 2015 ni kwamba hakuna mtu yoyote anaeruhusiwa kuvaa vazi hilo popote ndani ya Chad… Japo haijathibitika ni nani kahusika na Shambulio hilo, stori mpaka sasa kutoka Chad zinataja sana kundi la Boko Haram kutokana na kitendo cha nchi hiyo kuisaidia Nigeria kupambana na Kundi hilo la wapiganaji.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.