Headlines nyingi sana kuhusu China na ishu ya dawa za kulevya… Tumeshasikia nyingi kuhusu Sheria zao kali, zimeshasikika stori za watu waliokamatwa, wengine wananyongwa… leo kiko kingine kilichoripotiwa huko na hapa tayari kimenifikia.
Moja ya stori kubwa kwenye headlines leo inahusu ishu ya ongezeko la watu wanaitumia dawa za kulevya… Stori hiyo imeyafungua mengine kwamba kumbe mwaka 2014 idadi ya watumiaji wa dawa za kulevya iliongezeka ambapo watu 46,300 waliingia kwenye list ya watu wanaotumia dawa hizo China.
Ripoti ya China National Narcotics Control Commission ambao wanahusika na udhibiti wa dawa hizo, inaonesha wengi wao ni vijana ambao umri wao ni chini ya miaka 35.
Kwa sababu China wamejitahidi sana kuzuia dawa za kulevya kama Cocaine na Heroine kuingia ndani ya nchi yao, unaambiwa sehemu kubwa watu hao wanatumia dawa ambazo ni kemikali pamoja na vidonge na watumiaji wenyewe ni watu zaidi ya Milioni 1.4
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.