Hekaheka imeinasa hii ishu toka Msasani, Dar.. baba kamwadhibu mtoto lakini jinsi ambavyo ametoa adhabu hiyo imeonekana kama kuna watu hawajapenda, kamjeruhi kutokana na kumchaa na waya wenye makalio.
Mtoto huyo ana umri wa miaka 10, kapata adhabu hiyo kwa vile baba hajapenda kitendo cha mtoto wake kutofanya homework.
Mtoto amesema siku hiyo alitumwa na baba yake kwenda kununua mihogo, aliporudi alimkuta baba yake anakagua madaftari na kumuuliza kwanini hajafanya homework, pamoja na kujitetea baba hakumwelewa, alichukua waya na kumchapa kwenye makalio alafu akamfungia ndani.. baadae majirani walikuja kumwokoa.
Baba huyo ameshikiliwa na polisi katika kituo cha Oysterbay.. mtoto kachukuliwa na viongozi wa dawati la jinsia, mama wa mtoto huyo ametafutwa akasema aliamua kutoroka baada ya kuchoka kipigo kutoka kwa mume wake.
Isikilize hapa hekaheka yote kama ulipitwa.
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook naInstagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.