Hii sio mara ya kwanza kupata stori kutoka Kenya kuhusu pombe ya kienyeji kuua watu, imeingia kwenye headlines tena leo June 24 2015 ambapo watu saba wamefariki na wengine wamelazwa Hospitali baada ya kunywa na pombe ya kienyeji.
Baada ya kunywa pombe hiyo walianza kutetemeka na wengine wakashindwa kutembea, hii ikafanya watu wa Usalama kuingia mtaa mmoja baada ya mwingine katika Kaunti ya Kiambu, Kenya.
“Macho yalianza kuuma, nikaanza kuumwa na tumbo” >>> aliongea mmoja watu waliokunywa Pombe hiyo na kuzidiwa.
Mtu mwingine nae anasimulia; “Nilivyokunywa nilijisikia tu ulevi wa kawaida, baadae usiku nikajisikia kutetemeka”
Watu hao walikutwa wakiwa na hali mbaya pembeni ya barabara. Hizi ni pichaz na stori hiyo iko kwenye sauti niliyorekodi habari kutoka K24 TV.
Jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.