Matukio ya baadhi ya wasichana wa kazi kuwatesa watoto wa waajiri wao yamekua yakitokea mara kwa mara na mengi yanahusishwa na waajiriwa hao kuwanyanyasa wasichana hao ambao wengi hulipiza kisasi kwa watoto wakati wenyewe wakiwa wamekwenda kwenye majukumu yao ya kila siku.
Taarifa zimekuwa zikitolewa kila wakati kuhusu matukio kama hayo, na leo headlines zimehamia Dubai ambao msichana wa kazi aliamua kumnyonga mtoto wa bosi wake mwenye umri wa miezi 11 kwa kutumia mtandio kwa madai amenyimwa ruhusa ya kwenda kumzika mama yake mzazi.
Msichana huyo alifanya kitendo hicho baada ya bosi wake kuondoka kwenda kazini na baada ya kumaliza kumnyonga alimpigia bosi wake simu na kumtaarifu kuwa mwanaye anapumua kwa shida…baada ya muda mama huyo alirejea na kumkimbiza mtoto wake hospitali lakini alifariki masaa mawili baadaye.
Msichana huyo ambaye anakabiliwa na kesi ya mauaji aliwaambia waendesha mashtaka kuwa ni kweli amefanya tukio hilo baada ya kutopewa ruhusa ya kwenda kumzika mama yake.
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook naInstagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.