Klabu ya Manchester United imempa ruhusa beki Rafael Da Silva kuhama kwenye klabu hiyo baada ya kuitumikia kwa muda usiopungua miaka 6, na kinachoendelea kwa sasa ni kwamba klabu hiyo sasa imeanza rasmi mchakato wa kumpata mrithi wake.
Manchester United wameambiwa itawalazimu kulipa kiasi cha Pound Milioni 13 na bonus ya Pound Milioni 1.4 ikiwa wanataka kupata saini ya beki wa kulia wa timu ya Torino, Matteo Darmian.
‘The Red Devils‘ walituma ujumbe kwa Torino kuulizia namna ya kumsajili beki huyo ambaye anaichezea timu ya taifa ya Italia.
Rafael amekuwa akiwindwa na vilabu vya Fiorentina, Galatasaray na Napoli, wakiungana na vilabu vingine viwili katika Premier League ambao nao wanamtaka Mbrazil huyo.
Darmian ambaye ameshaichezea mara 13 timu yake ya taifa, ni miongoni mwa mabeki wa kulia ambao ni chaguo la kwanza la Louis Van Gaal.
Gregory Van der Wiel wa PSG, Seamus Coleman wa Everton na Fabinho wa Monaco nao wamemvutia Van Gaal katika kutafuta mrithi wa Rafael.
Gazeti la kiitaliano la Tuttosport limeripoti kwamba Manchester United wametuma ofa ya kwanza kwa ajili ya kumsaini Darmian, hata hivyo gazeti la Daily Mail limeripoti kwamba vilabu vya United na Torino ndio vimeanza mazungumzo.
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.