Kiungo wa kimataifa wa Rwanda anaekipiga katika klabu ya APR ya Rwanda Jean Baptiste Mugiraneza jana July 14 2015 amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea klabu ya Azam FC.
Kiungo huyo amesaini mkataba huo ikiwa ni siku mbili zimepita toka acheze mechi mbili za majararibio kati ya African Sport na Coast Union mkoani Tanga katika Uwanja wa Mkwakwani.
Hata hivyo ada ya uhamisho bado haijatajwa lakini inadaiwa atakuwa analipwa sio chini ya dola 4000/= kwa mwezi ambayo ni kama Tshs. Milioni nane.
Kufuatia kusajiliwa kwa kiungo huyo Azam FC itakuwa imebakiwa na nafasi moja pekee ya kusajili raia wa kigeni, ambapo shirikisho la soka Tanzania TFF linaruhusu kusajili wachezaji wakigeni wasiozidi saba.
Licha ya kusaini mkataba Jean atalazimika kurudi katika klabu yake ya APR na kuitumikia katika mashindano ya Kagame Cup yanayotarajia kuanza July 18 jijini Dar Es Saalam na baadae kujiunga rasmi na klabu ya Azam FC katika mashindano mbalimbali ikiwemo ligi kuu soka Tanzania bara.
Chanzo cha hii Stori >>> SALEH JEMBE
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook naInstagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.