Michuano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na kati Kagame CUP imeendelea leo kwa michezo kadhaa kupigwa. Michuano hiyo ambayo ina makundi matatu A, B na C. Timu za APR ya Rwanda na Azam FC ya Tanzania zimekuwa timu nyingine kusogea hatua moja mbele kwa kubeba ushindi kwenye Mechi zao za kwanza na kufuzu katika hatua ya Robo Fainali baada ya kushinda mechi za leo.
Azama FC iliyopo kundi C na timu za Adama City, KCC na Malakia imeshinda kwa jumla ya goli 2-0 dhidi ya Malikia ya Sudan Kusini, magoli yalifungwa na John Bocco dakika 27 na Kipre Tchetche dakika ya 52 hivyo Azam FC kutinga hatua ya Robo Fainali ya michuano hiyo kwa kuongoza kundi C kwa jumla ya point 6.
Hata hivyo APR ya Rwanda nayo imetinga hatua ya Robo Fainali ya michuano hiyo baada ya kuifunga Heegan kwa goli 2-0 na kuwa kinara wa kundi B kwa jumla ya point 6 nyuma ya LLB AFC.
Kwa matokeo hayo timu ya Azam FC itacheza mchezo wake wa tatu wa kukamilisha ratiba dhidi ya Adama City July 25 katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam huku klabu ya APR ya Rwanda itakamilisha ratiba kwa kucheza na LLB AFC July 23 Uwanja wa Taifa pia.
Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.