Rais wa Russia Vladimir Putin ni mmoja ya Marais ambao wana misimamo ya kipekee sana kwenye Uongozi wao.
March 2015 aligonga headlines za duniani baada ya kupitisha utaratibu mpya, aliamua kukata mshahara wa kila mfanyakazi wa Serikali mpaka wa kwake mwenyewe kwa 10% kutokana na hali ya Kiuchumi Russia kuwa mbaya!
Kingine kilichogusa headlines July 27 2015 ni ishu ya Rais Putin kuwasimamisha kazi Wafanyakazi 110,000 wa Wizara ya Mambo ya Ndani wa Nchi hiyo… hakuna sababu yoyote iliyotolewa kuhusu uamuzi huo lakini wengi wanahusisha uamuzi huu na ishu ya kuyumba kwa Uchumi wa Russia.
Idadi hiyo ya waliosimamishwa kazi ni kama 10% ya Idadi ya Wafanyakazi wote wa Idara hiyo ambayo ina Vitengo kama Wanajeshi, Polisi na Askari wa Usalama Barabarani.
Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.