Ujerumani ni moja kati ya nchi zinazofanya vizuri katika Ulimwengu wa soka lakini pia iliwahi kuandaa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2006… Sifa ya nchi hiyo sio tu kuandaa michuano mikubwa bali hata kuwa na viwanja vizuri kama Olympiastadion na Allianz Arena.
Allianz Arena ni uwanja wenye muonekano kama puto kwa nje na una uwezo wa kuingiza watu 69,901, una uwezo kuingiza watu wengi zaidi ya Uwanja wa Taifa Dar Es Salaam ambao unauwezo wa kuingiza watu 60,000 pekee. Umejengwa kwa euro milioni 340, uwanja huo ni miongoni mwa viwanja vilivyotumika katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2006.
Uwanja huu ambao upo mjini Munich Ujerumani hutumiwa kama uwanja wa nyumbani na vilabu vitatu vya mji huo, kama FC Bayern Munchen na TSV 1860 Munchen lakini kwa wakati mwingine hutumiwa na timu ya taifa ya Ujerumani,umekua pia kama kivutio kizuri kwa mashabiki wanaokwenda uwanjani hapo kutazama mechi kwani huwa unabadilika rangi kulingana na timu mwenyeji kwa siku hiyo atakuwa nani.
Ona pichaz na video za uwanja huo unavyobadilika rangi mtu wangu.
Cheki na Video yake hapa unavyobadilika badilika.
https://youtu.be/-sB8OAk5RyU
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos