Zikiwa zimebaki takribani siku 30 kabla ya dirisha la uhamisho barani ulaya kufungwa, hatma ya mchezaji Pedro katika klabu ya FC Barcelona nayo inakaribia kupata muafaka.
Pedro ambaye kwa muda wa wiki kadhaa sasa amekuwa akihusishwa na kujiunga na klabu ya Manchester United ambayo wanaripotiwa kuwa katika hatua za mwisho za kumuuza winga wake Angel Di Maria.
Jana Raisi wa FC Barcelona Josep Bartomeu alisema mpaka sasa hawajapokea ofa ya aina yoyote kwa ajili ya mauzo ya Pedro, lakini kwa mujibu wa mama mzazi huyo, Pedro atajiunga na klabu ya mojawapo nchini Uingereza: “Siku kadhaa zilizopita mama mzazi wa Pedro alisema kwamba mwanae atajiunga na klabu ya England”, – maneno haya yamezungumza na Jaime Lorenzo, Rais wa klabu ya Raqui San Isidro, jana usiku katika show ya Radio ya El Larguero. Raqui San Isidro ni klabu iliyomlea Pedro na kumfundisha soka.
“Nahisi utakuwa uhamisho mzuri kwa Pedro – ataenda mahala ambapo atapata nafasi zaidi ya kucheza. Klabu yetu itapata mgawo wa €400,000 kutoka kwenye kiasi kisichopungua €30m watakacholipwa Barca.
CEO wa United, Ed Woodward, anategemewa kusafiri kwenda Barcelona mapema wiki ijayo.