Ajali ambazo huripotiwa kila wakati nyingi ni zile zinazohusisha magari barabarani, lakini ajali za angani, majini na za treni hutokea lakini si kila wakati.
Huko India hakuishiwi matukio, kuna hii ajali nyingine imetokea usiku jana usiku baada ya treni mbili kukosea njia na mabehewa sita kutumbukia mtoni na kusababisha vifo vya watu 24.
Treni hizo zilitumbukia katika mto uliokuwa umejaa maji kutokana na mvua kubwa kuendelea kunyesha katika jimbo la Madhya Pradesh, na kusababisha idadi hiyo ya vifo na watu zaidi ya 300 kuokolewa.
Shirika la habari la India limesema ajali hiyo imetokana na treni hizo zilizopoteza mwelekeo kutokana na mafuriko.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos