Kila binadamu anapokuwa mdogo huwa na malengo au ndoto yaani ni namna ambavyo angependa kuwa wakati atakapokuwa mkubwa. Kila mtu utakayebahatika kukutana naye atasema mimi nataka kuwa hivi na mwingine akasema ningependa kuwa vile, sio kila ndoto au mipango tunayopanga huwa kama tulivyopanga.
August 5 nakuletea story ambayo team ya millardayo.com ilipata nafasi ya kumuuliza nahodha wa klabu ya Dar Es Salaam Young African na timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Nadir Haroub Cannavaro yeye kipindi yuko mdogo alitamani kuwa nani ni kweli mpira ilikuwa ni ndoto yake?
“Hayo mambo anakuwa anapanga mungu dream yangu mimi nilikuwa nataka kuwa mtu wa kawaida tu niwe askari lakini kila kitu anapanga mungu hata kwenye mpira nilikuwa napenda sana kuwa golikipa lakini nikawa central defender”>>>Cannavaro
Cannavaro alijiunga na Yanga mwaka 2006 akitokea katika klabu ya Tembo Sports klabu ya kutokea kwao visiwani Zanzibar.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos