Ubaguzini kitu ambacho kama ukikifanya alafu watu wakajua hivyo hakuna mtu atakuchukulia poa hata kidogo… imetokea mfululizo Marekani, Wamarekani weusi wameuawa na Maofisa Usalama na watu wakaingia Mtaani kulaani kwa nguvu, machafuko makubwa yakatiokea zaidi ya mara mbili !!
Dereva wa Taxi New York Marekani kaangukia mikononi mwa Sheria, kamgomea mama mmoja Cynthia Jordan na watoto wake wawili wa kike kuingia kwenye Taxi akawajibu kwamba muda wake wa kazi umeisha, hatua chache mbele akakuta watu wengine ambao ni wazungu wawili akawapakia akaondoka nao.
Mahakamani hawajachukulia poa hii kitu, dereva huyo wa taxi Baqir Raza kaambiwa alipe faini ya Dola Elfu 10 (Sawa na kama Tshs. Mil.20 hivi) kwa mwanamke huyo Cynthia Jordan na nyingine Dola Elfu 15 Mahakamani kwa kosa hilo, hukumu ambayo hata mwanamke aliyebaguliwa karidhika nayo kabisa.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos